SIYO WOTE WANAOSEMA "HUWEZI" WANAMAANISHA KWAMBA HUWEZI; WENGINE NI WIVU TU


Habari za leo, ndugu msomaji wa makala zangu za hamasa katika hatua za mafanikio katika biashara na ujasiriamali.


Namshukuru sana Mwenyezi Mungu, muumba wa mbingu na nchi. Aidha, napenda kukushukuru sana wewe msomaji wangu na nakuombea Mungu akufanikishe katika mambo yako yote na uwe na kibali kikuu katika kazi zako zote.​


Siyo wote wanaosema "huwezi" wanamaanisha kwamba huwezi kweli kufanikiwa; la hasha. Wengine wanasema hivyo kwa sababu ya wivu tu, wengine kwa sababu hawajui nguvu uliyonayo katika kufikia mafanikio; wengine kwa sababu hawana uelewa na mambo unayofanya; na wengine kwa sababu wana midomo ya kusemea.​


Ukitaka kupiga hatua na kufanikiwa katika maisha yako, acha kuambatana na wakatisha tamaa. Acha kukaa na kuwasikiliza watu wenye lengo la kukukatisha tamaa.​


Pia, katika kupiga hatua ya mafanikio, usisubiri sana watu waseme. Anza kupiga hatua huku ukijifunza kwa waliofanikiwa na kuangalia walifanikiwaje, na pia kujifunza kwa waliofeli ili ujue walifelije.​


Maneno mabaya huzorotesha nguvu ya kupiga hatua. Maneno mabaya yana nguvu kubwa sana katika kukurudisha nyuma kuliko maneno mazuri.​


KWA USHAURI, ELIMU NA UWEZESHAJI KATIKA HATUA YA URASIMISHAJI WA BIASHARA NA HUDUMA TANZANIA


Wasiliana nasi kupitia:​

Forbes


📞 +255 758 051 641

📧 mwahalendealfred@gmail.com​


Tutakusaidia kufikia malengo yako na kufanikiwa katika biashara yako.

Comments

Popular posts from this blog