MANENO YAKO, IMANI YAKO NA THAMANI YAKO VIMEKUFIKISHA HAPO ULIPO


#️⃣NA ALFRED MWAHALENDE KUTOKA ALFAKHA CONSULTING AGENCY LIMITED


#️⃣ Habari za leo ndugu msomaji wa makala zangu za hamasa katika hatua ya mafanikio kwenye biashara na Ujasiriamali.

#PowerYourbusiness2021 #AlfakhaconsultingAgency


👉 Maneno mabaya yanaua nguvu yako ya  kusonga mbele. Usikae na watu wanaokusemea mabaya wataua nguvu yako na kukunyong'onyesha hutapata nguvu ya kuamka kupiga hatua za mafanikio.

👉 Kuna wazazi hutamka maneno mabaya juu ya watoto wao utasikia mzazi anamwambia mtoto wake " Huna akili; wewe ni mbwa tu; Mbuzi tu; kilaza; zero Brain; Maneno haya huua Ndoto na matamanio ya watoto, huvunja mioyo yao na kuwafanya washindwe kupiga hatua. Maneno mazuri huwajenga watoto kutafuta kukufurahisha mzazi kwa kufanya mazuri unayowatamkia


#️⃣Leo naomba nikukumbushe jambo hili ambalo limeua Ndoto ya watu wengi na limewagharimu wengi bila kujua.


#️⃣ Maneno yako, Imani yako na thamani yako vimekufikisha hapo ulipo. Uko hapo kwa sababu ya maneno uliyojisemea au kusemewa. Maneno mazuri yanakupa nguvu ya kuchukua hatua zaidi. Maneno mabaya huzorotesha nguvu na ufanisi. Maneno mabaya yanaua ari ya kusonga mbele.


#️⃣ Hivi unajua maneno unayojitamkia au kutamkiwa ni zao na Hali uliyonayo Leo? Watu wengi wamekuwa wakijitamkia maneno mabaya " utasikia wanasema wa  "kufanikiwa awe Mimi" 

" Mimi maskini tu"

"Sina akili" Mimi ni mjinga tu " siwezi lolote "Ukoo wetu/familia yetu hatuwezi kufanya biashara" 


#️⃣ Maneno ya kujitamkia yanakufanya Ushindwe au ushinde Jambo lililopo mbele yako. Kama unakiri ushindi utashinda na Kama unatamka kushindwa utapokea kushindwa.


#️⃣ Maneno mabaya juu yako yanapunguza Imani uliyonayo kwenye kufikia mafanikio fulani, maneno mabaya huleta hali ya kukata tamaa.


#️⃣ Mafanikio huja kwa sababu ya nguvu na msukumo wako wa ndani kufikia hatua fulani. Kama unatamka kushindwa huwezi kupata Msukumo wa kupiga hatua.


#️⃣KWA USHAURI ELIMU NA UWEZESHAJI KATIKA HATUA YA URASIMISHAJI WA BIASHARA NA HUDUMA YAKO

+255758051641

mwahalendealfred@gmail.com

Comments